Caf imemfungia mechi 4 Hamari Traore.

Published from Blogger Prime Android App
CAF imemfungia mchezaji wa timu ya Taifa ya Mali beki Hamari Traoré mechi nne (4) kutokana utovu wa nidhamu dhidi ya Mwamuzi aliyechezesha mechi kati ya Ivory Coast na Mali katika mashindano ya kombe la AFCON.

Pia Shirikiso la Mali limetozwa faini ya Dola 10,000 huku kwa upande wa Ivory Coast wakipigwa  faini ya dola 5,000 kwa utovu wa nidhamu wakati wa mchezo.

Itakumbukwa kuwa Ivory Coast ndio waliotwaa Kombe la Afrika baada ya kuwachapa Nigeria kwenye fainali.

No comments:

Post a Comment